TAMSYA Yakutana na African Relief and Community Development

Na Iddy M. Kamana,
Ijumaa - Januari 16, 2026

Rais wa TAMSYA Br. Abdulhakim R. Abdallah ameongoza Viongozi waandamizi wa TAMSYA Makao Makuu Katika ziara rasmi alipo mtembelea Mkurugenzi Mkuu Bw. Mohammed Juweil, ofisini kwake.
Ziara hii maalumu ilijikita katika kuimarisha mahusiano kati ya TAMSYA na ARCD katika nyanja mbalimbali zitakazo wanufaisha Wanafunzi na Vijana wa Kiislamu nchini Tanzania. Taasisi ya ARCD, imekamilisha na kukabidhi Jengo Msikiti wa Kisasa, huko Mkoani Kigoma.

"TAMSYA inaendelea kuimarisha mifumo yake ya utambuzi wa Wanachama na kuboresha huduma zaidi Kwa vijana huku ikilenga zaidi Katika uwezeshaji wa Vijana kiuchumi" alisema Rais Abdulhakim R.
Vile vile Bw. Juweil, alisema "ARCD, itasaidia Jamii na itakuwa tayari kushirikiana na TAMSYA katika maeneo mbalimbali hasa eneo la huduma za mayatima"

Tunatumai mashirikiano yataleta fursa zaidi za Kwa mayatima na vijana kupitia mikopo laini na Uwezeshaji kiuchumi.