KIKAO KAZI TAMSYA na PBZ.

Uongozi wa Jumuiya ya wanafunzi na vijana wa kiislaam Tanzania (TAMSYA) Siku ya Alhamis ilifanikiwa kukutana na uongozi wa benki ya watu wa Zanzibar (PBZ BANK) tawi la Lumumba na kufanya nao mazungumzo yenye kulenga kuwa na ushirikiano katika utendaji wa majukumu mbalimbali ambayo yatakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Kwa upande wa TAMSYA waliongozwa na Rais wa Jumuiya ABDULHAKIM ABDALLAH aliyekuwa na Katibu Mkuu wa Br. JUMA JAPHARY, sambamba na viongozi waandamizi kutoka idara mbalimbali za TAMSYA TAIFA.

Aidha kwaupande wa PBZ BANK waliongozwa na Br. Rajabu Mohamad Ramia,Mkurugenzi wa PBZ Ikhlas na Viongozi waandamizi akiwemo Ukhty. Hikma Mohamed Meneja Tawi la PBZ Lumumba na Br. Mohammed.

Kwa umoja wao wote hao walizungumza juu ya namna gani wanaweza kushirikiana huku kila mmoja akiwa anatekeleza majukumu yanayomkabili bila kuathiri majukumu ya mwingine huku wakiwa na mustakabali mpana wakuwasaidia vijana na wanafunzi wa kiislamu Ili kuweza kufikia malengo waliyonayo.

Rais wa TAMSYA Br. Abdulhakim Abdallah,  amesema wapo tayari kushirikiana na PBZ BANK kwa namna yoyote Ile itakayokuwa na manufaa kwa vijana na wanafunzi wa kiislamu nchini kwani ndio walengwa wakuu wa jumuiya,
Aidha Rais wa TAMSYA na timu yake waliahidi kutoa ushirikiano Kwa Benk ya PBZ ili kuongeza huduma Kwa jamii katika maeneo ya usaidizi na uwezeshaji Vijana, Programu za Jumuiya, Elimu ya fedha na miamala ya Kiislamu.

Kwaupande wa PBZ wao wamesema wapo tayari kushirikiana na TAMSYA katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali, ambapo wamependekeza kwa pamoja TAMSYA na PBZ kuandaa Mkataba wa mashirikiano (MoU) katika maeneo mbalimbali yanayo leta mafanikio kwa pande zote mbili.

"Benk ya watu ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na TAMSYA katika kuhudumia Umma, hivi sasa hakuna dharula kwa waislamu kutumia huduma zisizofuata sharia, hivyo ni muhimu kufikisha elimu hii kwa Umma, Tuna amini TAMSYA ina Vijana wengi na ujumbe huu utafika kwa haraka katika Jamii" alisisitiza Mkurugenzi wa PBZ Br. Rajab Mohamed.