Hatua mpya ya kuimarisha malezi, elimu na maendeleo ya vijana wa Kiislamu imechukua sura mpya Morogoro Vijijini, baada ya TAMSYA kufanya kikao na BAKWATA kilichowakutanisha viongozi wa dini na wadau wa elimu kutoka kata zote sita.
Aidha Kikao hicho kimejumuisha Masheikh wa kata, Maimamu wa misikiti, wawakilishi wa madrasa pamoja na walezi wa shule za msingi na sekondari, kwa lengo la kujenga ushirikiano wa pamoja kwa mustakabali wa vijana.
Sambamba na hayo Kikao hicho kimekuwa jukwaa muhimu la kusikiliza na kujadili changamoto zinazowakabili vijana na wanafunzi wa Kiislamu, huku viongozi na wadau wakisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kizazi cha vijana kinapata malezi bora ya dini, elimu na maadili. Ushirikiano huo unatajwa kuwa nguzo muhimu katika kuimarisha maendeleo ya jamii ya Kiislamu Morogoro Vijijini.
Hata hivyo, Hatua hiyo imezua matumaini mapya kwa viongozi wa dini, walezi na wadau wa elimu, huku TAMSYA na BAKWATA zikieleza dhamira ya kuendeleza ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya vijana. Kikao hicho kimehitimishwa kwa msisitizo wa kuunganisha nguvu za viongozi wa dini, walimu na walezi ili kujenga vijana wenye elimu, maadili na uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya Taifa.
MWISHO
Imeandaliwa na Hanipha Haji
Idara ya Habari TAMSYA Mkoa wa Morogoro