Mkutano mkubwa wa vijana wa Kiislamu wa Afrika Mashariki ujulikanao kama East Africa Muslim Youth Conference, unaoandaliwa kwa ushirikiano wa jumuiya tatu kuu za vijana wa Kiislamu katika kanda yetu, ambazo ni: Tanzania (TAMSYA), Kenya (AMUCK), na Uganda (MSAU).
Mkutano huu unatarajiwa kufanyika tarehe 30/08/2025 Katika Ukumbi wa NSSF Mafao Houseukihusisha zaidi ya vijana na viongozi 200 kutoka vyuo vikuu, taasisi na jumuiya mbalimbali za Kiislamu kutoka nchi husika.
Malengo ya mkutano huu ni pamoja na, Kuimarisha mshikamano wa vijana wa Kiislamu wa Afrika Mashariki, Kukuza uongozi, umoja na mshikikano wa kijamii. Kujadili changamoto na fursa za kielimu, kiuchumi na kimaadili zinazowakabili vijana wa Kiislamu