Mkutano wa TAMSYA Pwani A uliofanyika novemba 23 katika chuo cha Kibaha Institute of Business.
Mkutano huo wajumbe mbalimbali waliweza kuhudhuria akiwemo kiongozi wa Taifa ambae alikuwa ni kaimu Naibu Katibu mkuu Br. Nurdiny Mtali, viongozi wa mkoa, wilaya, walimu walezi kuwakilisha baadhi ya wilaya, Viongozi wa TAMSYA kutoka mikoa jirani, Viongozi wa taasisi mbalimbali kama JAI na BAWAKITA mwakilishi kutoka Ofisi ya Sheikh wa Mkoa, mwakilishi kutoka ofisi ya Afisa Elimu wilaya ya Kibaha pamoja na mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
Miongoni mwa mambo yaliyofanyika ni pamoja na Semina ya uongozi, nasaha mbalimbali kutoka kwa wageni na viongozi wa taasisi pamoja usomaji wa ripoti ya utendaji na fedha ya TAMSYA Pwani A 2024.
Allah awalipe kheri sana wote mlioshiriki na azidi kutusimamia kuweza kufanikiwa kuiongoza Jumuiya mbele zaidi.